Rt. Rev. Eusebius Alfred Nzigilwa

Auxiliary Bishop of Dar-es-Salaam.

HISTORIA FUPI YA ASKOFU EUSEBIUS A. NZIGILWA

KUZALIWA

Alizaliwa Agosti 14 mwaka 1966, Mkoani Mwanza. Baba yake ni Alfred Nzigilwa (17 Aprili 1930)-alikuwa mfanyakazi katika shirika la Posta na Simu Tanzania, na alistaafu akiwa mfanyakazi wa shirika hilo makao makuu-Dar es Salaam; na Mama yake ni Roza Nzigilwa (30 Agosti 1935)-alikuwa ni Muuguzi, na alistaafu akiwa Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana-Dar es Salaam.

ELIMU

Alisoma shule ya Msingi ya Msimbazi Boys kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 1980. Alijiunga na Seminari ndogo ya Mtakaifu Petro iliyopo Jimbo Katoliki Morogoro kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita kuanzia mwaka 1981 hadi 1987 na baada ya kuhitimu kidato cha VI alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa OLJORO ARUSHA na Mgulani Dar es Salaam mnamo mwaka 1987 hadi mwaka 1988. Alisoma masomo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Kibosho mwaka 1988 hadi mwaka 1990. Alisoma masomo ya Teolojia katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo Kipalapala mwaka 1990 hadi mwaka 1995.

ELIMU YA JUU

Alisoma Shahada ya kwanza ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 1999- 2003 na Shahada ya pili ya Uzamili ya Utawala katika elimu mwaka 2008- 2010.

DARAJA TAKATIFU: UPADRE NA USHEMASI

Alipewa daraja ya Ushemasi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Januari 6 mwaka 1995 na Askofu Mkuu Polycarp Pengo na daraja ya Upadre Juni 23 mwaka 1995 katika viwanja vya Msimbazi Centre na Askofu Mkuu Polycarp Pengo.

KAZI ALIZOFANYA

Agosti 1995 – Desemba 1997 alikuwa mlezi katika nyumba ya malezi Kunduchi Mtongonaji. Desemba 1997 – Septemba 1999 alikuwa Gambera wa Seminari ndogo ya Mtakatifu Maria – Visiga. Agosti 1995 – Desemba 1997 alikuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Machi 1996 – Desemba 1997 alikuwa Mlezi wa Shirika la Utoto Mtakatifu, mwaka 1995 – 200 alikuwa Katibu wa Umoja wa Mapadri Jimbo Kuu la Dar es Salaam(UMAWADA) 2005 – 2009 Alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Mapadri Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

UASKOFU

Mnamo Januari 28, 2010 Baba Mtakatilfu Benedikto XVI alimtangaza kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Aliwekwa Wakfu kuwa Askofu Msaidizi katika viwanja vya Msimbazi Centre Machi 19, 2010.

Ni Askofu wa Jina wa Mozatcori.